Taarifa Kuhusu Huawei Health na Faragha

Mara ya mwisho kusasishwa: Oktoba 1, 2019

Huawei Health inatoa mfululizo wa vipengele vya ufuatilizi wa mazoezi, mbali na huduma za afya na ukufunzi mahiri wa mazoezi. Programu hii inahitaji kuunganisha kwa Intaneti wakati wa matumizi, na inahitaji kufikia vipengele au vibali vifuatavyo: Eneo, Bluetooth, Kamera, Maikrofoni, Wasiliani, Rekodi za nambari za simu, Simu, na Hifadhi. Pia inahitaji kukusanya na kusindika maelezo yafuatayo:

• Maelezo ya mtandao na kifaa, yakiwemo kitambuaji kifaa, mipangilio ya kifaa, mipangilio ya kibinafsi, anwani ya IP na aina ya mtandao.

• Maelezo ya kibinafsi, yakiwemo Kitambulisho chako cha HUAWEI na kimo na uzito wako, ambayo yataisaidia programu hii itoe data sahihi zaidi.

• Data ya mazoezi, ikiwemo eneo la kifaa, njia, aina na muda wa mazoezi, hali ya kukimbia, idadi ya hatua, masafa, kalori, mwinuko uliotimizwa, VO2 max, na mpigo wa moyo wa mazoezi. Data hii itakusanywa kwa lengo la kuhifadhi na kuonyesha.

• Data ya afya, ikiwemo usingizi, mpigo wa moyo, mfadhaiko, na asilimia ya mafuta mwilini kwa malengo ya kuhifadhi na kuonyesha.

Data yako ya mazoezi na afya inajumuisha maelezo nyeti ya kibinafsi. Njia ambayo data hii inatumia – ikiwemo kama inapakiwa au haipakiwi kwenye Huawei Health Cloud, pahali inapopakiwa, na inadhibitiwa na nani – inang'amuliwa kulingana na eneo lako, nchi/eneo unalochagua, au maelezo ya kuingia kwenye akaunti unayotoa. Ili kupata maelezo zaidi, nenda kwenye Mimi > Mipangilio > Mipangilio ya faragha.

Programu hii itafanya kazi tu ukikubali ukusanyaji wa maelezo ya hapo juu na kutoa vibali vinavyohitajika. Ili kukomesha ukusanyaji na usindikaji wa maelezo ya hapo juu, na kunyima vibali ulivyotoa, sakinusha programu au nenda kwenye Mimi > Mipangilio > Mipangilio ya faragha na zima ubadilishaji wa maelezo ambayo hutaki kuyagawiza.

Onyeshazaidi